HOME

Jan 19, 2012

MTOTO HUYU ANAHITAJI MSAADA WAKO AWEZE KUPONA!!

Huo hapo jichoni ndio uvimbe mkubwa unaomsumbua mtoto Josephat


Mtoto Josephat mwenye umri wa miaka 16 ana tatizo la uvimbe mkubwa kwenye jicho ambao umetunga usaha na kumsababishia kutoona kabisa kwani kila anavyozidi kukua na uvimbe huo unazidi kuongezeka.


Kwa mujibu wa maelezo yake Josephat amesema tatizo hilo limemuanza tangu akiwa mtoto na hajawahi kupatiwa msaada wowote kwasababu hana ndugu wala mahali pa kuishi na sasa hivi ana tangatanga mitaani baada ya kutoka Dodoma alipokuwa akiishi katika kituo cha basi.


Mtoto huyu amefika leo mchana katika Ofisi EATV/EA Radio akiomba msaada wa matibabu kuhusiana na tatizo hilo ambalo hajui hatma yake itakuwa nini na kiukweli nimejisikia vibaya sana kwani hali yake ni mbaya sana huwezi kumuangalia mara mbili au hata mara moja kama una roho nyepesi tafadhali kama una uwezo msaada wako ni muhimu sana kwakuwa yeye mwenyewe hakupenda ni mipango ya Mungu,Hapo alipo hajui atakula nini wala atalala wapi.TUSAIDIANE!!!


Kama umeguswa na hali ya mtoto huyu na unahitaji kumsaidia kwa njia yoyote ile,Tafadhali tuwasiliane kupitia email marygorethrichard@gmail.com.

No comments:

Post a Comment