HOME

Jan 20, 2012

RAIA WA UINGEREZA AFA KWA KUNG'ATWA NA NYUKI AKIWA KWENYE SHUGHULI ZA UTALII NCHINI!!

Kamanda Adolphina Chialo

Raia mmoja wa nchini Uingereza Michael Brian (61) amefariki dunia baada ya kung’atwa na nyuki.


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Bi Adolphina Chialo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho majira ya saa 12 jioni Januari 19 mwaka huu  huko katika kijiji cha Mangayi melela wilayani Mvomero ambapo marehemu
huyo alikuwa kwenye shughuli za kiutalii.


Hata hivyo chanzo cha kung’atwa na nyuki hao hakijafahamika na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ukisubiri taratibu zaidi.

No comments:

Post a Comment