HOME

Jan 26, 2012

JULIANI AWATETEA MASHABIKI!!

Juliani















Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Juliani kutoka Kenya, ambaye amejizolea mafanikio makubwa hivi karibuni, amewashauri wasanii wenzake kupunguza matarajio yao makubwa waliokuwa wamejiwekea kwenye kuvuna kipato, na kuwa wepesi katika bei wanazoweka kwa ajili ya kufanya maonyesho.


Kwa mujibu wa msanii huyu, wadau wa burudani wanatakiwa kuchukuwa muda huu kukuza majina yao na kushirikiana na mashabiki wao kwa karibu kama wana matumaini ya kujipatia biashara katika kipindi hiki.


Juliani amejipangia kutumia mwezi huu mzima wa Januari kutembelea shule mbalimbali na makanisa katika kufanya huduma na kugawa album yake mpya aliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana inayofahamika kama ‘Kawaida ya Maisha’.

No comments:

Post a Comment