HOME

Jan 23, 2012

RAIS KIBAKI AAGIZA KUUNDWA TIMU YA WANASHERIA KUFUATIA UAMUZI WA ICC!!

Rais Mwai Kibaki akihutubia taifa la Kenya.


















Rais Mwai Kibaki amelihutubia taifa jioni hii baada ya kutolewa uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu ICC kwamba watuhumiwa wanne kati ya sita wa vurugu za uchaguzi wana kesi ya kujibu.


Rais Kibaki amemuagiza mwanasheria mkuu wa serikali kuunda timu ya wanasheria kuishauri serikali jinsi ya kushughulikia suala la kesi ya wathumiwa wa vurugu kufuatia uamuzi ulitolewa na mahakama ya ICC.


Pia amewataka na kuwasisitiza wananchi wa Kenya kuwa watulivu na kusonga mbele kulijenga kwani jukumu lake ni kuhakikisha nchi hiyo ipo katika amani na utulivu. 

No comments:

Post a Comment