HOME

Jan 30, 2012

HUDUMA MAHOSPITALINI ZAENDELEA KUWA MBAYA!!

Madaktari walio kwenye mgomo

Hali ya huduma za afya katika zahanati na vituo vya afya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ni mbaya kutokana na madaktari kuendelea na mgomo wao usio na kikomo licha ya waziri mkuu Mizengo Pinda jana kuwataka madaktari hao kuacha mgomo na kurejea kazini kuanzia leo.


Hii leo Madaktari hao wamesaini vitabu vya mahudhurio na kuondoka huku wakiacha idadi kubwa ya wagonjwa wakiwa hawana mtu wa kuwatibu hali inayotishiwa kutokea kwa vifo.


Katika kitengo cha dharura cha hospitali ya taifa Muhimbili, hali ni mbaya baada ya magari ya kubeba wagonjwa maarufu kama ambulance, kulazimika kugeuza na wagonjwa mahututi kutokana na kutokwepo kwa madaktari.

No comments:

Post a Comment