HOME

Jan 22, 2012

WATU KADHAA WAMEUWAWA KATIKA SHAMBULIO NIGERIA!!

















Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa kwenye milipuko iliyotokea katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria.


Vituo vya Polisi pamoja na makao makuu ya Polisi eneo hilo ni miongoni mwa sehemu zilizolengwa katika mashambulizi hayo.


Milio ya risasi pia imesikika katika sehemu kadhaa ambapo kundi la kiislamu la Boko Haram limesema ndilo lililotekeleza mashambulizi hayo.


Kundi hilo ndilo limekuwa likifanya vurugu katika siku za hivi karibuni, kwenye eneo la kaskazini mwa Nigeria, lililo na Waislamu wengi.

No comments:

Post a Comment