HOME

Jan 30, 2012

BEYONCE KUJENGEWA SANAMU NYUMBANI KWAO!!


Baada ya kutawala na kufanya vizuri katika soko la muziki ikiwa ni pamoja na kupata tuzo kibao kutokana na kazi zake nyota wa Muziki ulimwenguni Beyonce au mama Ivy Blue anatarajia kupata kitu ambacho hajawahi kupata.

Mji wa nyumbani kwao alikozaliwa wa Houston,Texas nchini Marekani unapanga kujenga sanamu kubwa la nyota huyo.

Kampuni ya masoko ya Armdeonce Ventures kwa kushirikiana na makampuni ya umma na binafsi yatagharamia ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwaka ambapo wafadhili hao wataweka majina yao katika sanamu hiyo na kulipia mapato yatakayotolewa kwa waathirika wa Kimbunga cha Katrina na wa mafuriko katika miji ya Tennessee,Alabama na Mississippi.

No comments:

Post a Comment