HOME

Jan 29, 2012

WAFUASI 11 WA BOKO HARAM WAUWAWA NIGERIA!!


Jeshi la polisi nchini Nigeria limesema kuwa limewapiga risasi na kuwauwa wafuasi 11 wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.


Msemaji wa jeshi hilo ameeleza kwamba wapiganaji hao waliuwawa wakati wa mapambano katika mji wa Maiduguri, ambako kundi hilo lilianzishwa muongo mmoja uliopita.


Juma lilopita takribani watu 185 waliuwawa katika mji mwingine wa Kano kaskazini mwa Nigeria kwenye mashambulio kadhaa ya mabomu.

No comments:

Post a Comment