HOME

Jan 31, 2012

WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MUHIMBILI!!

Waziri wa Afya Dk. Haji mponda

Habari za hivi punde ni kuwa  Waziri wa Afya Dk. Haji mponda amefanya  ziara ya kushtukiza katika hospitali ya taifa ya muhimbili na Taasisi ya mifupa ya muhimbili (MOI)  kufuatilia utendaji.

Akizungumza na waandishi wa habari Dk Mponda amesema mpaka sasa ametembelea baadhi ya maeneo na kuainisha kuwa huduma zinaridhisha.

Aidha ameeleza kuwa sehemu inayosuasua ni emergency department, ambapo madaktari kutoka jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) wamewekwa kuziba maeneo ya wazi.

Nae mkurugenzi wa MOI Prof Laurence Museru amesema katika taasisi hiyo wanaendelea kujitahidi kuhudumia wagonjwa kulingana na namba ya  Specialist 30 walioko kazini

No comments:

Post a Comment