Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa bado kwenye mgomo katika viwanja vya hospitali hiyo Dar es Salaam wakati madaktari wa jeshi wakiletwa hospitalini hapo kutoa huduma. |
Kikosi cha madaktari kumi na tano kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo kimepelekwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kutoa huduma baada ya waliokuwa madaktari katika hospitali hiyo kuwa katika mgomo usio na kikomo na uliosababisha huduma za afya kuzorota.
Baadhi ya madaktari hao wamekuwa wakitoa huduma katika kitengo cha wagonjwa wa dharura, ambapo kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Bw. Aminiel Aligaesha, madaktari wengine wanatarajia kuwasili hospitalini hapo kutoka wizara ya Afya pamoja na taasisi nyingine zinazotoa huduma za Afya.
No comments:
Post a Comment