HOME

Jan 24, 2012

RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI KUITWA MAHAKAMANI!!

Rais Barack Obama



















Jaji wa mahakama katika jimbo la Georgia nchini Marekani ametoa hati ya kuitwa mahakamani rais Barack Obama wiki hii kufuatia shauri lililofunguliwa mahakamani ambalo linahoji ikiwa Obama ni mzaliwa halisi raia wa Marekani mwenye sifa za kuwa rais wa nchi hiyo.


Kesi hiyo imefunguliwa katika mahakama hiyo na kundi la wanaharakati linalojiita "birther" ambalo linadai kuwa haijawekwa wazi ikiwa rais Obama alizaliwa nje ya nchi, na mkazi mwingine wa  Georgia  amefungua madai ambayo anataka jina la Obama liondolewe katika kura za jimbo hilo wakati wa uchaguzi wa awali wa rais utakaofanyika mwezi Machi.


Hata hivyo haiko wazi ikiwa mahakama inaweza kumlazimisha rais aliyeko madarakani kuhudhuria mwenendo wa kesi ambapo kaimu jaji kiongozi wa mahakama hiyo Michael Malihi amekataa hoja ya mwanasheria wa rais ya kutaka kufuta hati hiyo ambayo inamtaka Obama kufika mahakamani.

No comments:

Post a Comment