Utafiti wa miaka minne kuhusu mafua ya ndege uliofanywa katika hospitali sita nchini Tanzania , umebaini kuwepo vimelea vya ugonjwa huo.
Utafiti huo umefanyika katika hospitali za mikoa ya Dodoma, Mwanza, Kigoma, Dar es Salaam na Manyara, zikiwemo za Wilaya ya Kibondo, Mwananyamala, Haidom na ya International School of Tanganyika (IST) iliyoko Dar es Salaam.
Mratibu wa Mpango wa Kukabiliana na ugonjwa huo, Elbanka Mwakapeje amesema mpango huo unalenga kuukabili ili usidhuru rasilimali watu, mimea na wanyama ambapo katika utafiti huo, Mwakapeje amesema watu 771 waliripotiwa kuwa na vimelea na kati yao mmoja alifariki dunia.
No comments:
Post a Comment