Jan 20, 2012
WANAWAKE WASUMBULIWA KWA KUVAA 'SURUALI' NCHINI MALAWI!!
Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika amesema wanawake wa nchi hiyo wako huru kuvaa vyovyote wanavyotaka.
Rais Mutharika ametoa kauli hiyo baada ya polisi kulikamata kundi la watu waliomvua nguo mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa suruali.
Katika hotuba aliyoitoa kupitia Radio inayomilikiwa na serikali , rais Mutharika amesema wanawake nchini humo wako huru kuvaa wanavyotaka ikiwa ni pamoja na kuvaa suruali na kuwahakikishia kuwa watalindwa dhidi ya wahuni na magaidi.
Rais Mutharika amesema alishangazwa na watu wa mtaani kuwabughudhi wanawake kwa kuvaa suruari wakati ni vazi ambalo linamlinda mwanamke kuliko kuvaa sketi,kauli hiyo ni ya kwanza ya rais Mutharika kuitoa wakati wanawake wanajiandaa kuandamana katika mitaa ya Blantyre leo kutetea haki ya kuvaa suruari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment