Moja ya Migodi ya dhahabu iliyopo hapa nchini Tanzania |
Wachimbaji wanne wa kata ya Gunyoda wilayani Mbulu mkoani Manyara wamefariki dunia huku wengine watatu wakinusurika kifo baada ya kuangukiwa na miamba ya mawe na shehena ya udongo kwenye mto Uderi wakati walipokuwa wakichimba madini ya dhahabu katika mto huo unaoaminika kugundulika kwa madini hayo.
Kwa mujibu wa Kaimu Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mbulu Bw. Leonard Tlatlaa amekiri kupokea miili minne iliyoopolewa na wananchi wa kata hiyo huku akieleza sababu ya vifo hivyo kuwa imetokana na wachimbaji hao kukosa hewa na baada ya kufunikwa na miamba ya mawe na udongo.
Daktari Tlatlaa amewataja waliopokelewa katika hospital hiyo kuwa ni Raphael Bombo,Baha Nade,Andrew Diamet na Titus Aloyce mwenyeji wa mji mdogo wa Haydom ambapo bado miili hiyo imehifadhiwa katika chumba maiti kusubiri ndugu na taratibu za maziko.
Kwa upande mwingine mmoja wa wachimbaji hao aliyenusurika kifo ameeleza sababu kubwa inayowasukuma kukiuka marufuku ya kutochimba dhahabu inayotolewa na viongozi wao wa kata na wilaya kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment