Jan 23, 2012
WAHAMIAJI HARAMU WA KISOMALI WAFIKISHWA MAHAKAMANI!!
Wamahamiaji haramu 98 wenye asili ya Kisomali pamoja na madareva wawili wa kitanzania wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoani morogoro wakikabiliwa na shtaka la kuingia nchini bila kibali wakitokea Handeni Tanga kuelekea mpakani mwa Mbeya kwenda nchi za jirani Malawi na Afrika kusini
Akisoma shtaka hilo Mbele ya hakimu mahakama ya hakimu mkazi mkoani Morogoro mwendesha mashtaka wa idara ya uhamiaji Hermin Foya amesema raia haowalikamatwa eneo la Melela njia panda ya Kilosa baada ya lori lililobeba wasomali hao lenye Namba za usajili 718 lilokuwa likiendeshwa na Emil Kimaro na John Masaka kuharibika.
Aidha amesema hii ni mara ya tatu kwa madereva hao kupatikana na hatia za kusafirisha wahamaiaji haramu kwenye lori la mizigo kinyumbe na sheria za magari ya mizigo huku na wasomali hao wakIingia nchini na kusafiri bila kuwa na kibali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment