Na. Mwandishi Wetu.
Baadhi ya mawakala wa pembejeo za ruzuku wasio waaminifu wilayani Ludewa katika mkoa mpya wa njombe wamekuwa wakiuza pembejeo hizo kinyume na utaratibu wa kawaida uliowekwa na serikali huku baadhi yao udanganyifu katika aina za mbegu wanazouza kwa kubadili majina halisi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma amebaini hayo katika ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika wilaya za Njombe na Ludewa ambapo katika kijiji cha Mlangali mkuu huyo wa mkoa alitembelea baadhi ya maduka ya pembejeo na kubaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na mawakala hao.
Baadhi ya watendaji wa vijiji na mawakala waliohojiwa kuhusiana na suala hilo wamekiri kukiuka utaratibu wa kawaida wakugawa vocha hizo kwa seti kama ilivyoagizwa na serikali kwamaelezo kuwa vocha hizo zimechelewa kufika katika maeneo husika ambapo wakulima walio wengi wameshapanda mahindi hivyo kutohitaji mbolea zakupandia pamoja na mbegu na badala yake wanahitaji mbolea aina moja tu ya urea kwaajili ya kukuzia tu.
Akiwa katika ziara yake ya siku sita katika wilaya za Njombe na Ludewa Dk. Ishengoma amekutana na mawakala wa pembejeo wa wilaya zote mbili na kuwaagiza kufanya kazi kwa uaminifu na akisisitiza kuwa serikali haitashindwa kuwalipa mawakala wazalendo watakaotoa huduma hiyo kwa wakulima huku mbunge wa jimbo la Ludewa Bw. Deo Philikunjombe akisema kuwa suluhu ya uchakachuaji huo wa pembejeo ni serikali kupeleka huduma hiyo mapema tofauti na sasa ambapo vocha hizo zinachelewa sana
No comments:
Post a Comment