Mwenyekiti wa soko hilo Bw. Aboubakar Rakesh akitangaza uamuzi huo leo katika mkutano uliowajumuisha wafanyabiashara wa jengo la soko hilo |
Mfanyabiashara katika jengo la Machinga Complex akiwa amepumzika baada ya kupungua wateja. |
Viongozi wa soko la Machinga Complex jijini Dar es salaam wameamua kuanzisha mbinu mbadala za kuwavutia wateja baada ya soko hilo kudorora na kukosa wateja kwa muda mrefu tangu kuanza kwa shughuli za biashara septemba saba mwaka 2010.
Akitangaza uamuzi huo leo katika mkutano uliowajumuisha wafanyabiashara wa jengo la soko hilo, mwenyekiti wa soko hilo Bw. Aboubakar Rakesh amesema wameamua kufikia uamuzi huo kutokana na uongozi wa Manispaa ya Ilala kutozingatia maoni yao juu ya utaratibu mbadala wa kuliboresha soko hilo.
Mbinu hiyo ni kuanzisha gulio sokoni hapo kila Jumamosi na Jumapili ili kuwavutia wateja ambapo watafanya mnada wa vitu na bidhaa mbalimbali zinazopatikana sokoni hapo.
No comments:
Post a Comment