Chalz Baba (kushoto),Zembwele na meneja wa chalz katika kipindi cha SuperMix Leo asubuhi. |
Mwanamuziki nguli wa dansi nchini Chalz Baba ambaye hivi karibuni amejitoa katika bendi ya Twanga Pepete leo anatarajiwa kutambulishwa katika bendi mpya aliyohamia ya Mashujaa band akiwa tayari amekamilisha wimbo na Bendi hiyo unaokwenda kwa jina la ''Ungenieleza''
Chalz Baba amezungumza na blog hii na kusema kilichomuondoa Twanga Pepeta si kingine bali ni maslahi aliyokuwa akiyapata na hakuna kingine kama watu wanavyozungumza na kusema hakuwa na mkataba na Twanga hivyo hata wakitaka kumshtaki kwa madai ya kukiuka mkataba wao waje na kushahidi na vielelezo vyote vitakayothibitisha suala hilo.
Pia amesema malengo yake kimuziki ni kuja kuwa na bendi yake binafsi na yeye aje kuitwa 'Mkurugenzi' ingawa kwa sasa ameamua kujiunga na mashujaa ambao wamempokea vizuri na kufurahia uwepo wake katika bendi hiyo.
No comments:
Post a Comment