Naibu Jaji Mkuu aliyefukuzwa kazi Nancy Baraza |
Rais Mwai Kibaki wa Kenya jana amemsimamisha kazi Naibu Jaji Mkuu Nancy Baraza na kuunda jopo ambalo litafanyia uchunguzi mwenendo wake kutokana na shutuma zinazomkabili.
Jopo hilo litaongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Augustino Stephen Lawrence Ramadhan kama Mwenyekiti.
Jaji Baraza, anashutumiwa kumtishia maisha kwa bastola mlinzi wa duka moja kubwa, Bi Rebecca Kerubo wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
No comments:
Post a Comment