HOME

Jan 30, 2012

SAKATA LA MGOMO WA MADAKTARI LACHUKUA SURA MPYA!!


Hali ilivyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili katika wodi za wagonjwa hapo ni mlangoni kama unavyoona hakuna huduma zinazotolewa hospitalini hapo kufuatia mgomo wa madaktari.


















Sakata la mgomo wa madaktari nchini Tanzania linazidi kuchukua sura mpya baada ya wataalamu hao kukataa hoja za ujumbe wa Serikali ulioongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi, Hawa Ghasia huku wakigoma kusikiliza kauli yoyote kutoka kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda.

Uamuzi huo umekuja waakati mawaziri hao wakikumbwa na tafrani ambapotayari wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na ile ya Mkoa wa Dodoma wametishia kusitisha utoaji huduma ifikapo Jumatatu kama masuala yao hayajapatiwa ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment