Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai (kulia) na mkurugenzi wa mashtaka ya ummaKeriako Tobiko wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. |
Serikali ya Kenya imesema kuwa naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta na mkuu wa utumishi wa ummaFrancis Muthaura hawatashinikizwa kujiuzuru licha jya uamuzi uliotolewa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu ICC kwamba wana kesi ya kujibu na shinikizo la wananchi wa Kenya kuwataka wajiuzuru.
Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai amesema maafisa hao wawili wa serikali wana nafasi ya kukata rufaa ya uamuzi huo na hawatahitajika kujiudhuru hadi watapotekeleza haki yao ya kukata rufaa.
Naibu waziri mkuu na mkuu wa utumishi wa umma ni moja kati ya watuhumiwa wanne ambao mashtaka yao ya uhalifu dhidi ya binadamu yalithibitishwa na ICC jana.
No comments:
Post a Comment