Ban Ki-moon |
Jengo jipya la Umoja wa Afrika lililopo mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa |
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amewataka viongozi wa kiafrika kuheshimu haki za mashoga.
Bw. Ban ameuambia mkutano wa umoja wa Afrika kuwa Ubaguzi wa kijinsia umekuwa haushughulikiwi na hata kuwekewa vizuizi na nchi nyingi kwa muda mrefu.
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria kwa nchi nyingi za kiafrika hali iliyopelekea kuongezeka kwa kashfa kutoka kwa wanaharakati na nchi za Magharibi.
Mkutano wa siku mbili unaofanyika katika jengo jipya la Umoja wa Afrika lilipo mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa unatarajia kuteua mwenyekiti mpya wa tume ya umoja wa Afrika.
No comments:
Post a Comment