HOME

Jan 16, 2012

WIZARA YA AFYA KUTOA TAMKO KUHUSU HATUA YA MADAKTARI KUIPA SERIKALI SAA 72!!

Bi Blandina Nyoni























Wizara ya afya na ustawi wa jamii Tanzania kesho itatoa tamko kuhusu hatua ya chama cha madaktari kuipa serikali muda wa saa 72 kuwarejesha kazini madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo katika hospitali ya taifa Muhimbili.


Katibu mkuu wizara ya ya, Bi Blandina Nyoni amesema hayo leo kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na onyo hilo ambapo amesema kwa sasa wanajadili hatua za kuchukua kabla ya kuziweka wazi kwa umma hapo kesho.


Mgogoro baina ya serikali na chama cha madaktari umeibuka baada ya serikali kushindwa kuwalipa madaktari hao posho zao za miezi miwili ya Novemba na Disemba mwaka jana, posho ambazo zililipwa mwanzoni mwa mwezi huu

No comments:

Post a Comment