HOME

Jan 30, 2012

NOVAK DJOKOVIC BINGWA AUSTRIAN OPEN!!

Novak Djokovic

Novak Djokovic kutoka Serbia, Jana alimshinda Rafael Nadal kutoka Uhispania, katika fainalil ya mashindano ya tennis ya Australian Open, iliyofanyika mjini Melbourne.


Djokovic anaendelea kuwa mchezaji wa kiume nambari moja ulimwenguni Djokovic alipata ushindi wa 5-7, 6-4, 2-6, 6-7, 7-5.


Pambano hilo sasa limeandikishwa katika historia kama shindano ambalo limechukua muda mrefu zaidi katika historia ya mashindano ya tennis ya Open.


Ushindi huo wa tatu mfululizo katika mashindano ya Grand Slam, umemchukua Djokovic muda wa saa tano, na dakika 53.


Pambano hilo limeandika historia pia kwa kuwa pambano la muda mrefu zaidi kwa mchezaji mmoja kwa mmoja katika mashindano ya Australian Open.

No comments:

Post a Comment