HOME

Jan 19, 2012

THEO ZWANZIGER AWATAKA WACHEZAJI MASHOGA KUJITOKEZA!!

Theo Zwanziger

Rais wa shirikisho la soka Ujerumani anayeondoka madarakani amesema umefika wakati kwa wachezaji wa soka ambao ni mashoga kujitokeza hadharani.


Theo Zwanziger, ambaya anategemea kuachia ngazi mwezi Machi amewataka wachezaji hao kuwa na ujasiri wa kujitangaza vile hasa walivyo, japo amekiri kuwa kuna ugumu wa kufanya hivyo.


Zwanziger amemtolea mfano meya wa jiji la Berlin, Klaus Wowereit, ambaye alijitokeza hadharani miaka iliyopita.


Akizungumza mada hiyo katika mjadala uliowekwa mezani na shirikisho hilo, Theo amesema kwa wachezaji mashoga wenye nia ya kujitokeza, wasiwe na wasiwasi kwani kwa sasa jamii inaelewa vema mambo hayo tofauti na miaka iliyopita.


Kepteni wa Ujerumani, Philipp Lahm, kwa upande wake hakubaliani kabisa na suala hilo.

No comments:

Post a Comment