Mkazi wa kijiji cha Ibebu kata ya Mwangudo wilayani Meatu Mkoani Simiyu nchini Tanzania Ibese Doto (40) amefariki dunia baada ya kukanyagwa na Tembo akiwa shambani kwake akilinda mazao yake yasiharibiwe na ndege na wanyama.
Kaimu kamanda wa polisi Mkoani Shinyanga amewaambia waandishi wa habari kuwa marehemu huyo akiwa shambani kwake mara ghafla alitokea Tembo huyo na kuanza kumshambulia na baadaye kumkanyaga hadi kuuuwa.
Kaimu kamanda huyo amesema kundi kubwa la Tembo limevamia katika kitongoji hicho likitokea kwenye hifadhi ya akiba ya pori la Maswa hali aliyodai inahatarisha maisha ya wananchi.
Amesema jeshi la polisi mkoani humo bado linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na namna gann ya kuweza kakabiliana kundi hilo kubwa la Tembo waliovamia katika maeneo hayo na hivyo kuwataka wananchi kujihadhari nao.
No comments:
Post a Comment