HOME

Jan 30, 2012

MBUNGE JANUARY MAKAMBA KUWASILISHA HOJA BINAFSI KATIKA BUNGE LINALOANZA KESHO!!

Mhe. January Makamba

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli nchini Tanzania January Makamba amesema anatarajia kuwasilisha hoja binafsi mbili katika bunge linaloanza kesho ikiwamo ya muswada wa sheria ya kudhibiti upangaji wa nyumba na muswada wa sheria ya kuwalinda watumiaji wa huduma za kifedha.


Akizungumza jijini Dar-Es-Salaam, Mbunge huyo wa Bumbuli amesema amelazimika kufanya hivyo kwa sababu karibia asilimia 60 ya wakazi wa mjini wanaishi katika nyumba za kupanga ambapo zaidi ya asilimia 40 ya mapato ya wananchi wanayatumia kulipia kodi za nyumba.


Amesema kukosekana kwa sheria kunawafanya wenye nyumba wajione wana haki bila ya wajibu, na kunapotokea majanga kama vile mafuriko au moto wapangaji hupoteza kila kitu na hawapati fidia huku serikali ikiwafidia wenye nyumba.

No comments:

Post a Comment