Rais Yoweri Museni (kusoto) akimtunikia nishani ya hesima rais Paul Kagame wa Rwanda |
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewatunukia nishani za heshima ya juu ya 0rder of the Pearl of Africa, the Grand Master marais wa Rwanda Paul Kagame na Theodore Obiang Nguema Obasago wa Equatorial Guinea.
Viongozi hao wametunukiwa nishani hiyo ya juu kwa mchango wao walioutoa wa amani na utulivu siyo kwa nchi zao tu bali hata kwa nchi nyingine za Kiafrika.
Sherehe hizo zilifanyika jana zikiambata na sherehe za maadhimisho ya miaka 26 ya chama cha NRA/NRM zilizofanyika katika chuo cha SebeiTegres katika wilaya ya Kapchorwa na sherehe hizo zilihudhuriwa na wake wa viongozi hao.
No comments:
Post a Comment