Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale kupitia CCM Wilayani Geita Hussein Nassor Amar |
Wananchi hasa waishio Vijijini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuhoji pale wanapokuwa na mashaka juu ya utekelezaji wanaotakiwa kuufanya kuepuka kugeuzwa shamba la Bibi kwa kugeuzwa vyanzo vya mapato yasiyo halali kutoka kwa baadhi ya watumishi wasio waadilifu hasa pale linapohusu fedha.
Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale kupitia CCM Wilayani Geita Hussein Nassor Amar amesema hayo jana kwa nyakati tofauati akiwa katika siku yake ya tatu ya kutembelea jimbo lake kuhamasisha na kukagua utekelezaji wa shuhghuli za miradi ya maendeleo aliokuwa anajibu baadhi ya kero kutoka kwa wananchi.
Akiwa katika kata za Kharumwa,Nyugwa,Izunya,MwingiroKakora na Nyabulanda kwa nyakati tofauti wananchi walihoji uhalali wa ulipiaji baadhi ya huduma za serikali pasipo kupewa stakabadhi za malipo wakihofia kwa fedha hizo kuhujumiwa kwa kutoingizwa serkalini.
Baadhi ya malipo hayo walidai kwua ni pamoja na malipo ya shilingi 1,000 kwa kila mfugo unaochanjwa wakiwemo Ng'ombe,Mbuzi na Kondoo kwa kukusanywa mamilioni ya fedha lakini hakuna mfugaji anayepewa stakabadhi lakini wanapohoji hutishiwa kukamatwa na maafisa wanaoendesha zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment