HOME

Jan 31, 2012

SERIKALI KUUNDA SERA YA KUWA NA CHOMBO KIMOJA CHA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA!!

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge, mh. wiliam lukuvi Bungeni mjini Dodoma.

Serikali ya Tanzania ipo katika  mchakato wa kuunda sera itakayowezesha kuwa na chombo kimoja cha kupambana na tatizo la matumizi na uingizwaji wa dawa za kulevya nchini.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge, mh. wiliam lukuvi ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Matembwe Mh. Kheri Ameir aliyetaka kujua ukubwa wa tatizo la matumizi ya dawa ya kulevya kitaifa na mipango ya kukabiliana nayo.

Mh. Lukuvi amesema, baada ya serikali kukaa vikao mbalimbali na kubaini kuwa na kitengo cha kuratibu mapambano dhidi ya dawa za lulevya, pamoja na jeshi la polisi kuwa na kitengo cha kupambana na dawa hizo sasa imeamua kuwa na kitengo kimoja ili kuongeza ufanisi.

Amesema hatua za kuundwa na chombo hicho ipo katika ngazi za juu za kitaifa kutokana na kutambua tatizo la matumizi ya dawa za kulevya katika takwimu za mwaka 2000 -2010 ambazo zimeonyesha kiasi cha dawa za kulevya kilichokamatwa na idadi ya watuhumiwa kuongezeka.

No comments:

Post a Comment