HOME

Jan 29, 2012

WAZIRI MKUU PINDA LEO ATAKUTANA NA MADAKTARI WALIO KWENYE MGOMO!!

















Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda leo Jumapili atakutana na madaktari jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kupata suluhu ya mgomo wao usiokuwa na kikomo.


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi ya waziri mkuu imesema kuwa Mhe. Pinda atakutana na madaktari hao katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa nne kamili asubuhi.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo madaktari hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiomba kuonana na waziri mkuu na mara zote amekubali kuonana nao lakini hawakutokea.

No comments:

Post a Comment