Kamishna wa polisi Hafiz Ringim |
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amemfukuza kazi kamishna wa polisi kutokana na kuongezeka kwavitendo vya mashambulizi yanayofanywa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram.
Hatua hiyo inakuja wiki chache za mashambulizi ya mfululizo ya kundi la Boko Haram yalifanywa hivi karibuni katika mji wa Kano siku ya Ijumaa ambapo watu 185 wamekufa.
Kundi hilo la Boko Haram limesema kuwa linataka kuuondoa utawala wa serikali ya Nigeria na kuingiza utawala wa kiislamu.
Taarifa kutoka ikulu ya Nigeria imesema kuwa Hafiz Ringim amelazimishwa kwenda likizo ya lazima huku akisubiri kustaafu rasmi.
Hatua ya kumtimua kazi mkuu wa polisi inaonekana kuwa ni njia mojawapo ya kuwafanya wa Nigeria wawe na imani na kikosi cha polisi cha nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment