HOME

Jan 30, 2012

TWIGA STARS YAIFUNDISHA KAZI NAMIBIA!!

Mshambuliaji Asha Rashid ''Mwalala' akifanya mashambulizi


Mabao mawili mawili kutoka kwa washambuliaji Asha Rashid ‘Mwalala’ na Mwanahamisi Omari ‘Gaucho’, jana yaliiwezesha timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, kuwachapa wenzao wa Namibia kwa kwa mabao 5-2, hivyo kuwatoa kwa jumla ya mabao 7-2 na kutinga raundi ya kwanza kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake (AWC), mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa.


Twiga iliyopewa nguvu ya kukabiliana na changamoto hiyo na mchango wa sh mil. 10 kutoka kwa ‘Marafiki wa Twiga’ kundi linaloundwa na wabunge wa Bunge la Tanzania na kiasi kama hicho kutoka Bohari ya Dawa Nchini (MSD), ililianza pambano hilo kwa kasi na uchu wa kuibuka na ushindi.


Harakati za Twiga zilizaa matunda dakika ya 21, ilipopata bao la kwanza kupitia Mwanahamisi Omari ‘Gaucho’, aliyeitendea haki krosi ya Asha Rashidi Mwalala, aliyeunasa mpira kutoka kwa beki Pulkeria Chalaji, aliyeanziwa fupi na mlinda mlango Fatuma Omari, kabla ya Namibia kuja juu na kusawazisha dakika ya 30.

No comments:

Post a Comment