HOME

Jan 6, 2012

ZAHOUI AKATAA OMBI LA MAN CITY

Francois Zahoui


Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast Francois Zahoui amekataa ombi la klabu ya Manchester City la kutaka ndugu wawili katika timu hiyo Yaya na Kolo Toure kucheza dhidi y mahasimu wao wakubwa timu ya Manchester United kombe la FA.


Zahoui ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa vilabu vinafahamu sheria na anawatarajia wachezaji hao kuutii utaratibu wa (Fifa),chini ya utaratibu wa (Fifa) wachezaji wanatakiwa kuitwa wiki mbili kabla ya michuano ya mataifa ya Afrika kuanza January 21.


City ilikuwa na matarajio ya ndugu hao wangeweza kucheza dhidi ya mashetani wekundu mechi ya jumapili kombe la FA kabla ya kujiunga na kambi ya timu ya Ivory Coast.

No comments:

Post a Comment