HOME

Jan 6, 2012

WAPANGAJI WA MAKAMBINI WATAKIWA KUHAMA!

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecky Sadiq


Waliokuwa wapangaji wa nyumba zilizobomolewa na mafuriko yaliyolikumba jiji la Dar es Salaam takribani wiki mbili zilizopita, ambao hivi sasa wanaishi katika kambi za muda, wametakiwa kuondoka katika kambi hizo ifikapo saa kumi na mbili jioni leo.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecky Sadick ametoa agizo hilo ofisini kwake leo ambapo amesema hatua hiyo inalenga kuzipa mamlaka husika nafasi ya kuandaa mazingira kuruhusu wanafunzi kuanza masomo pindi shule zitakapofunguliwa jumatatu ijayo.


Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, serikali haihusiki na hasara walioyoipata watu hao kwani sio iliyowatuma watu hao kupanga katika maeneo yasiyo salama.


Ameonya kuwa nguvu huenda zikatumika kuwaondoa watu hao kwani serikali ilishatoa muda wa kutosha kwa wahanga hao kutafuta na kwamba kwa sasa inashughulika na wahanga ambao walikuwa na nyumba katika maeneo yaliyoathiriwa.

No comments:

Post a Comment