HOME

Jan 12, 2012

SHEREHE ZA MAPINDUZI

Balozi Seif Ali Idd

Watanzania leo wanaungana na Wazanzibari kusherehekea miaka 48 ya mapinduzi  ya Zanzibar ambapo sherehe zake zinafnyika katika Uwanja wa amani huku rais wa  Zanzibar Dk. Alli Mohamed Shein akitarajiwa kulihutubia taifa


Akizungumza  na wandishi wa habari makamu wa pili wa rais wa Zanzibar ambaye  ndie mwenyekiti wa kamati ya sherehe hizo Balozi Seif Ali Iddi amesema maandalizi yote yamekamilika na rais wa Zanziabr Dk. Ali Mohamed Shein atalihutubia taifa baada ya kupokea mandamano ya wananchi na gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama huku rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakya Kikwete naye akiwa anahudhuria sherehe hizo.


Serikali ya mapinduzi inatarajiwa kutumia shilingi milioni mia saba kufanikisha sherehe hizo ambazo ni kubwa kwa Zazibar zikiwa ndio siku ambayo utawala wa  kifalme uliondolewa na wananchi wa Zanziabr waliongozwa na jemedari rais wa kwanza wa Zanziabr marehemu Abeid Amani Karume.

No comments:

Post a Comment