HOME

Jan 12, 2012

MWANDISHI WA HABARI AUWAWA KATIKA VURUGU NCHINI SYRIA!!

Vurugu zinazoendelea katika mitaa mbalimbali Syria

Gilles Jacquier
Mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Ufaransa Gilles Jacquier ameuwawa katika mji wa Homs nchini Syria ambapo anakuwa mwandishi wa kwanza wa nchi za Magharibi kuuwawa katika vurugu zinazoendelea nchini humo.


Kituo cha Televisheni cha Ufaransa kimesema mwandishi huyo wa habari alikuwa katika safari ya kiserikali kwenye mji huo ambapo kituo cha televisheni cha Syria kimesema Jacquier alikuwa ni moja kati ya watu nane waliouwawa.


Mwandishi mwingine wa habari amesema kuwa dakika chache zilizopita walitoka kuwafanyia mahojiano watu kadhaa katika makusanyiko ambapo makundi ya upinzani yamesema watu 24 wamekufa katika maeneo mbalimbali ya nchi hapo jana wakiwemo watu 10 kutoka mji wa Homs.


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo Alain Juppe ametaka maelezo ya kutosha juu ya kilichotokea.

No comments:

Post a Comment