HOME

Jan 12, 2012

MFUNGWA AWAUWA WAFUNGWA WENZIE KATIKA GEREZA LA KAMITI NCHINI KENYA!!

Kamiti Prison
Wafungwa wawili katika gereza lenye ulinzi wa hali ya juu la Kamiti nchini Kenya wameuwawa hapo jana na mfungwa mwingine ambaye anatumikia kifungo cha maisha jela.


Mfungwa huyo Christopher Njoroge,anayedaiwa kusumbuliwa na matatizo ya akili amedaiwa kuwauwa wafungwa wenzake kwa kuwaumiza vibaya ambapo mmoja alikufa papo hapo na mwingine alikufa kutokana na majeraha makubwa aliyopata akiwa katika hospitali ya Kenyatta.


Mfungwa huyo anayetumikia kifungo cha maisha kwa kushtakiwa na Jamhuri alidaiwa kuonyesha dalili za kuugua ugonjwa wa akili kabla ya kutenda tukio hilo ka kushtusha.


Naibu kamishna mkuu wa magereza  Benjamin Njoga amesema wanasubiri taarifa za kikao ili kuelezea mazingira halisi yaliyosababisha vifo vya wafungwa hao wawili ambao pia walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha na kuongeza kuwa watawasiliana na familia za marehemu hao katika kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment