Ditto |
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ditto amesema hakutegemea kama wimbo wa ''Tushukuru kwa yote'' utawateka watu kiasi ambacho umeweza kuwateka hivyo hadi sasa haamini kinachotokea kikubwa anamshukuru mungu na mashabiki wake popote walipo duniani
Ditto amefunguaka kuwa ''mipango yangu kwa mwaka 2012 mashabiki wajiandae kununua albam yangu online pia tunaanza mchakato wa kumalizia website yangu''
Pia amesema ''kingine muhimu zaidi mwezi huu naanza kushoot documentary itakayohusu maisha yangu binafsi na ya muziki watayajua mengi ambayo hawakuwahi kuyajua kupitia documentary hiyo''
No comments:
Post a Comment