HOME

Jan 10, 2012

SERIKALI IMEWASAMEHE WANAFUNZI DARASA LA SABA WALIOFUTIWA MATOKEO.

Mhe. Philipo Mulugo


Serikali ya Tanzania imewasamehe wanafunzi 9,629 wa darasa la saba waliofutiwa matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana, baada ya kubainika kuwa na majibu yenye kufanana kusiko kwa kawaida.




Hata hivyo watahiniwa 107 waliofutiwa matokeo kwa kukutwa na majibu hawakupewa msamaha hivyo wataendelea na adhabu hiyo na waliosamehewa sasa watarudia mitihani hiyo wakati wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwezi septemba mwaka huu.




Akizungumza jijini Dar-Es-Salaam, Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo amesema serikali imechukua uamuzi huo baada ya kupokea maoni na malalamiko kutoka kwa wazazi, walezi, jamii na wadau wengine wa elimu nchini.

No comments:

Post a Comment