HOME

Feb 3, 2012

BUNGE HALINA MGUSO NA WANANCHI ‘OUT OF TOUCH’


Inasikitisha kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala mbalimbali bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta Afya. Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali kuhusu mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa. Bunge likaahirishwa siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipohitaji taarifa ya Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo walifanya ujanja ujanja kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari.


Leo wabunge kwa mara nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa dharura. Naibu Spika wa Bunge akatumia sababu za kiufundi kuzuia mjadala. Inawezekana wabunge hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga mkono hoja, lakini ni jukumu la Kiti kuona umuhimu na udharura wa mijadala.ENDELEA HAPA

No comments:

Post a Comment