HOME

Feb 10, 2012

MWANAMKE ATELEKEZWA NA MUMEWE BAADA YA KUJIFUNGUA MAPACHA WATATU!!


Mwanamke mmoja jijini Kampala jana amebaki katika mshangao mkubwa baada ya baba wa vijacha vyake vitatu alivyojifungua katika hospitali ya Mulago kupotea baada ya kupata taarifa hizo.


Mwanamke huyo Hawa Namaganda wa mji mdogo wa Kampala,Masajja Zone B amejifungua watoto mapacha watatu Ijumaa iliyopita lakini alipata mshtuko baada ya mume wake Abdu Balinnya ambaye alikuwa anamjali wakati wote wa ujauzito kupotea baada ya kupokea taarifa hizo kwa njia ya simu.


Vichanga hivyo vitatu vya kike vilivyoongeza idadi ya watoto wake kufikia wanne ambapo mtoto wake wa kwanza Rajab Kasule ana umri wa miaka saba.

No comments:

Post a Comment