HOME

Feb 5, 2012

HASSANALI KUIWAKILISHA TANZANIA BANGALORE!!


Mbunifu maarufu wa mavazi nchini Tanzania, Mustafa Hassanali amealikwa nchini India kushiriki wiki ya mitindo ya Bangalore iliyoanza nchini humo.


Maonyesho hayo ambayo ni mara ya pili kushiriki kwa mbunifu huyo yatampa nafasi ya kutangaza utamaduni wa Tanzania pamoja na kuonyesha kipaji cha ubunifu alichonacho.


Onyesho hilo la Bangalore ni tukio lake la 24 la kuonyesha ubunifu wa mitindo akiwa tayari ameshafanya hivyo katika nchi za Sweden, Botswana, Angola, Afrika Kusini na Niger.

No comments:

Post a Comment