HOME

Feb 3, 2012

WAVUVI WATAKIWA KUACHA KUTUMIA ZANA HARAMU.


Wavuvi nchini  Tanzania wametakiwa kuacha kutumia zana haramu za uvuvi  kwasababu zinasababisha kuvua samaki wadogo na  kuangamiza wengine ambao wangeweza kukuwa na kuongeza pato la nchi.


Hayo yamesemwa na Meya wa manispaa ya Singida Alhaji Salumu Mahami wakati alipokuwa akichoma moto makokolo na neti ya mbu zenye matundu madogo zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi  wa bwawa la Singida kuvulia samaki kinyume na sheria.


Mahami amesema kitendo cha kuvua samaki  wakiwa bado wadogo kinalikosesha taifa fedha nyingi, kwahiyo amewaomba wananchi na wavuvi  kushirikiana na wataalamu wa uvuvi   iliwaweze kufuata sheria za uvuvi  kwa ajili ya manufaa ya taifa.

No comments:

Post a Comment