HOME

Feb 23, 2012

SOMALIA KUJADILIWA LONDON!!


Tishio la ugaidi na uharamia ni miongoni mwa masuala yatakayo jadiliwa katika mkutano huo wa London kuhusu hatma ya Somalia.


Wawakilishi kutoka nchi 40 watahudhuria mkutano huo wenye lengo la kutafuta suluhu juu ya matatizo yanayoikumba nchi hiyo kufuatia miongo miwili ya vita na ukame.


Viongozi wanatarajiwa kukubaliana kuhusu pesa za ujenzi wa shule, hospitali na idara ya polisi.


Uingereza imeielezea Somalia kama nchi iliyoporomoka zaidi duniani lakini imesema kuna haja ya kuipa Somalia nafasi nyingine ili iweze kuibuka kutoka matatizo yake.


Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali, ambaye ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria mkutano huo ameonya kuwa nchi yake iko katika njia panda na inahitaji usaidizi mkubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment