HOME

Feb 3, 2012

SERIKALI YAKANUSHA GADAFFI KUWEKEZA NCHINI!!


Serikali ya Tanzania imesema aliyekuwa rais wa Libya marehemu Kanali Muammar Gaddafi hakuwahi binafsi kuwekeza kibiashara hapa nichni.


Akijibu swali la Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi, aliyetaka kujua Tanzania inanufaika vipi na uwekezaji wa kanali Muammar Gaddafi kibiashara, na kwa kuwa Tanzania haitambui serikali ya mpito ya Libya ni nani anayesimamia uwekezaji wa kibiashara wa marehemu kanali Muammar Gaddafi.


Akijibu hoja hizo, waziri  wa nchi ofisi ya waziri mkuu, uwekezaji na uwezeshaji, mh Mary Nagu amesema kwa mujibu wa kumbukumbu za kituo za uwekezaji zinaonyesha mradi mmoja tu ulioandikishwa kutoka  Nchini Libya na kampuni ya NORTH AFRICA INVESTMENT TRADING COMMPANY  na si wa marehemu kanali Muammar Gaddafi.


Amesema kampuni hiyo imeandika andiko la kibiashara la kuwekeza jumla ya dola za kimarekani milioni 5.8 na kutengeneza nafasu za ajira 160 ambapo ilinunua hotel ya bahari beach  ya
jijini dar es salaam.

No comments:

Post a Comment