HOME

Feb 17, 2012

RAIS KIKWETE KUZINDUA MRADI WA NG'OMBE!!


Rais Jakaya Kikwete kesho anatarajia kuzindua mradi wa serikali wa uwezeshaji wa wafugaji unaolenga kuwasaidia wafugaji   walioko katika wilaya za longido, monduli na ngorongoro mkoani arusha waliopoteza mifugo yao yote kutokana na ukame wa mwaka 2008/2009.


Serikali iliamua kuwapatia wafugaji waliopoteza ng’ombe wao katika vipindi hivyo viwili kama kifuta jasho kutokana na ukame liosababisha mifugo mingi kufa


Mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo ameeleza katika kuashiria uzinduzi  wa mradi huo Rais kikwete atakata utepe katika mnara uliojengwa kwa ajili ya mradi huu wilayani Longido  pamoja na kukabidhi mitamba na madume bora kwa baadhi ya wafugaji.


Amesema hatua ya  wananchi hao kupewa mitamba na madume bora ni moja ya mikakati ya Rais Kikwete ya kuhimiza wananchi kufanya mageuzi katika sekta ya ufugaji ili waweze kufuga kisasa

No comments:

Post a Comment