Khulekani "Mgqumeni" Khumalo |
Mtu mmoja nchini Afrika Kusini anayedai kuwa ni mwanamuziki mashuhuri aliyekufa, anashikiliwa na mamlaka za nchi hiyo hadi watakapothibitisha utambulisho wake kwa vipimo vya DNA, wamesema polisi.
Mtu huyo anasema yeye ni Khulekani "Mgqumeni" Khumalo - mwanamuziki wa nyimbo za kiasili za Kizulu ambaye alifariki mwaka 2009 ambapo alizuka katika nyumba ya familia yake wiki iliyopita akidai kuwa alikuwa ametekwa na mizuka.
Familia yake wakiwemo wake zake wawili, wanasema anaonekana kuwa ndio mwenyewe - lakini polisi wamesema atashtakiwa kwa udanganyifu iwapo vipimo vya DNA vitaonesha anadanganya.
No comments:
Post a Comment