HOME

Feb 8, 2012

KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE KUKUTANA JUU YA MGOMO WA MADAKTARI!!

Naibu spika wa bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai

Naibu spika wa bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai  ameiomba kamati ya uongozi ya bunge kukutana mara moja ili kujadili namna bunge litakavyowezesha kutoa kauli kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea hapa nchini.


Maamuzi hayo ya naibu spika yamekuja kufuatia mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Peter Selukamba kuongezea idadi ya wabunge waliowasilisha hoja ya dharura kutaka bunge kujadili mgomo wa madaktari unaoendelea na kusababisha vifo vya watanzania kutokana na kukosa huduma.


Akizungumza kabla ya kuhitimisha sehemu ya kwanza ya kipindi cha maswali na majibu Naibu spika wa bunge Mh. Job Ndugai amesema kutokana na mbunge kusimama kwa mara ya saba amesema ni vigumu kwa bunge kuendelea kukaa kimya kwa suala hilo.

No comments:

Post a Comment