Feb 23, 2012
WABUNGE KENYA WAOMBOLEZA KIFO CHA WAZIRI WA MAZINGIRA!!
Wabunge wa bunge la Kenya jana wameahirisha shughuli za bunge mara mbili kuomboleza kifo cha waziri wa mazingira John Michuki ambaye amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo Jumanne usiku.
Bunge hilo kwa mara ya kwanza liliahirisha shughuli zake asubuhi na mchana wakati wabunge walipokuwa wakimzungumzia Bw. Michuki kama kiongozi mkweli na shujaa wa taifa hilo.
Rais Kibaki jana aliagiza bendera kupepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo ambapo baadae jioni makamu wa rais Kalonzo Musyoka,spika wa bunge Kenneth Marende na wabunge kadhaa waliitembelea familia ya Bw. Michuki huko Ridgeways jijini Nairobi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment